Harare. ZANU PF kuwaadhibu wasaliti.
4 Septemba 2005Matangazo
Chama tawala nchini Zimbabwe kimekana ripoti za vyombo vya habari kuwa kinatayarisha orodha ya watu wanaoikosoa ambao watapigwa marufuku kusafiri kwenda nje ya nchi chini ya sheria mpya zilizopitishwa na serikali hiyo.
Chama cha rais Robert Mugabe cha Zanu PF kimetumia wingi wake bungeni wiki iliyopita kuidhinisha mageuzi ambayo yataruhusu serikali kutaifisha mashamba ambayo hapo kabla yalikuwa yakimilikiwa na wazungu na kuweka vikwazo vya kusafiri kwa wale wanaoonekana kuwa ni wasaliti.