1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE. Zimbabwe imo hatarini kufukuzwa kutoka IMF

2 Septemba 2005

Zimbabwe iko katika hatari ya kufukuzwa kutoka shirika la fedha duniani IMF.

Shirika la fedha Duniani limesema Zimbabwe ina malimbikizi ya madeni yaliyopindukia hata ingawa nchi hiyo imelipa kiasi cha dola milioni 120 kupunguza deni hilo kubwa.

Kamati ya Shirika la fedha duniani itakutana tarehe 9 septemba kujadili juu ya hatua ya kuifukuza Zimbabwe ambayo imeshindwa kulipa deni lake tangu mwaka 2000 kwa sababu za kutokuwa na fedha za kigeni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW