HARARE Zimbabwe yabomoa makazi ya mabanda
23 Juni 2005Matangazo
Zimbabwe inaendelea na hatua yake ya kuyabomoa makazi ya mabanda mjini Harare. Zaidi ya watu elfu 42 wamekamatwa au mali yao kuchukuliwa katika operesheni hiyo ambayo imezusha hasira katika jamii ya kimataifa. Hata hivyo polisi nchini humo inasema operesheni hiyo tayari imesaidia kupunguza uhalifu kwa karibu asilimia 20 tangu ilipoanza mapema mwezi Mei.
Rais Robert Mugabe anasema hatua hiyo ni muhimu kuwakamata wahalifu ambao wamevigeuza vitongoji vya mji kuwa masoko ya biashara haramu. Marekani, Uingereza na umoja wa Ulaya zimeikosoa hatua hiyo ya rais Mugabe, ambayo imeulazimu umoja wa mataifa kumtuma mjumbe wake maalumu kuchunguza hali halisi.