1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Zimbabwe yapuuza ripoti ya Umoja wa Mataifa

27 Julai 2005

HARARE: Zimbabwe yapuuza ripoti ya Umoja wa Mataifa

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Anna Tibaijuka amemuambia kuwa alishinikizwa kutoa ripoti kali kuhusika na ubomoaji wa nyumba na vibanda vya biashara vilivyojengwa kinyume na sheria nchini Zimbabwe.Gazeti la „Herald” linalodhibitiwa na serikali,limemnukulu Mugabe akisema kuwa Tibaijuka alipokuwepo Zimbabwe alimueleza kwamba katika tume yake ya uchunguzi,walikuwepo watu kuhakikisha kuwa ripoti inalaani vikali.Serikali ya Harare imeipuuza ripoti ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuwa inapendelea upande mmoja na si ya haki.Serikali ya Mugabe imetengwa na mataifa ya magharibi hasa kwa sababu ya mradi wa mageuzi ya ardhi uliozusha mabishano na pia madai kuwa imefanya udanganyifu wa uchaguzi tangu mwaka 2000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW