HARARE:Kanisa katoliki Zimbabwe lalaumu serikali
31 Agosti 2007Matangazo
Maaskofu wa kanisa la katoliki nchini Zimbabwe wanalaumu serikali kwa kujaribu kufumbia macho mkwamo wa kisiasa na kiuchumi kwa kupigia debe madai ya unzizi dhidi ya Askofu mkuu Pius Ncube.Bwana Ncube ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Mugabe.
Mkutano wa maaskofu wa kanisa katoliki walimsifu Askofu Ncube kwa dayosisi ya Bulawayo kwa ujasiri wake,uadilifu na ukosefu wake wa woga wa kufichua mauaji yaliyosababishwa na majeshi ya serikali wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 80 vilevile wakati wa operesheni ya kubomoa mitaa ya mabanda mjini Harare mwaka 2005.