1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Kesi ya uhaini ya Tsvangirai yaanza tena

3 Desemba 2003
Kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morga Tsvangirai ambaye anatuhumiwa kula njama za kumuuwa Rais Robert Mugabe imeanza tena hapo jana kwa siku moja tu baada ya kuahirishwa kwa miezi minne huku mawakili wa serikali wakitaka kuongezwa kwa mashtaka dhidi ya yake. Tsvangirai anashtakiwa kwa madai ya kupnmga njama za kumuuwa Mugabe kabla ya uchaguzi wa Rais wa mwezi wa Machi mwaka 2002 ambapo kiongozi huyo wa upinzani alishindwa na Mugabe. Wakili wa serikali Joseph Musakwa amemwambia hakimu Poddington Garwe kwamba wanataka kurekebisha madai ya mashtaka kwa kujumuisha mazungumzo ya maandalizi ya serikali ya mpito na kutafuta uungaji mkono wa kijeshi baada ya kuuwawa kwa Mugabe.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW