HARARE.Rais Mugabe aidhinisha mabadiliko ya katiba
31 Agosti 2005Matangazo
Rais Robert Mugabe wa zimbabwe ameidhinisha marekebisho yaliyofanyiwa vifungu kadhaa vya katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo wakosoaji wamesema kwamba vifungu hivyo vinampa uwezo zaidi rais Mugabe wa kuweza kuitawala nchi hiyo.
Wabunge wa Chama cha ZANU PF cha rais Mugabe waliowengi katika bunge wameiidhinisha mabadiliko hayo ambayo yatairuhusu serikali kuyataifisha mashamba ya wazungu pamoja na kuweka vikwazo vya usafiri kwa watu wanaotajwa kuwa wasaliti.
Chama cha Mugabe kinadai mabadiliko hayo yataiwezesha serikali kumaliza mzozo wa ardhi chini ya mpango wa marekebisho ya umiliki wa ardhi ambapo utawezesha mashamba ya wazungu kugawanywa kwa wakulima weusi.