HARARE:Robert Mugabe kugombea tena urais kwa tiketi ya ZANU-PF
6 Mei 2007Matangazo
Chama tawala nchini Zimbabwe kimesema rais Robert Mugabe atawania kipindi kingine cha miaka 6 cha urais kwa tiketi ya chama cha ZANU PF.
Afisa wa ngazi ya juu kwenye chama hicho Diydus Mutasa amesema chama chao kimeutatua mzozo wa kuwania madaraka kwa kumuunga mkono rais Robert Mugabe.
Kwa muda sasa chama hicho tawala kimekuwa na mgawanyiko kuhusu suala la uongozi.
Diydus amenukuliwa akisema chama cha ZANUPF kimekubaliana hakiwezi kumuondoa rais Robert Mugabe kwani anahitajika na chama pamoja na taifa kwa jumla ambalo linakabiliwa na matatizo.