HARARE:Serikali ya Mugabe yakosolewa na kundi la madhehebu ya wakatoliki wa Zimbabwe
20 Juni 2005Matangazo
Kundi la madhehebu ya wakatoliki limeishutumu serikali ya rais Robert Mugambe kwa hatua ya kuyavunja makaazi ya mabanda na kusababisha watu wapatao laki mbili kukosa makazi ya kuishi.
Tume ya sheria na amani ya kanisa katoliki nchini humo imesema kampeini hiyo ya Mugabe ya kuisafisha nchi imezidisha matatizo ya maskini wengi wa Zimbabwe ambao tayari wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula.
Askofu Pius Ncube ameikosoa serikali hiyo na kuilaumu kwa ukosefu wa uongozi bora wa mzozo wa kiuchumi nchini Zimbabwe.
Maafisa wa serikali wanadai ukame wa muda mrefu ndio chanzo cha kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa chakula lakini wakosoaji wanailaumu hatua ya mugabe ya kuyachukua kwa nguvu mashamba ya wakulima wazungu nchini humo.