1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris aelezea kujitolea kwake kuiunga mkono Israel

26 Julai 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ameelezea kujitolea kwake kusikoyumba kwa Israeli kufuatia mkutano na waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu.

Kamala Harris
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala HarrisPicha: Kaylee Greenlee Beal/REUTERS

Harris anayetarajiwa kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba nchini Marekani, ametoa wito kwa uongozi wa Israel kuchukuwa hatua zaidi kuwalinda raia katika Ukanda wa Gaza. 

Kiongozi wa Hamas katika ukingo wa Magharibi afariki akiwa kizuizini Israel

Harris ameongeza kuwa Israel ilikuwa na haki ya kujilinda na kwamba alimueleza Netanyahu kuhusu wasiwasi wake mkubwa juu ya kiwango cha mateso ya binadamu huko Gaza yanayojumuisha vifo vya raia wengi wasiokuwa na hatia pamoja na hali mbaya ya kibinaadamu.

Makamu huyo wa Rais pia amesema hawawezi kupuuza majanga hayo na wakati huo huo akatoa wito kwa raia wa Marekani kutilia maanani utata wa mgogoro huo na historia ya eneo hilo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW