1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris aunguruma Michigani, Trump yupo majimbo ya maamuzi

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Mgombea Urais wa chama cha Democratic Kamala Harris anafanya kampeni yake katika jimbo la Michigan leo, huku mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump akiwa katika majimbo matatu ya maamuzi upande wa mashriki.

Uchaguzi Marekani 2024 | Kamala Harris - Donald Trump
Wagombea wa rais Marekani Kamala Harris - Donald TrumpPicha: AP/picture alliance

Wagombea wote wawili wanakabiliwa na kinyang'anyiro kikali katika majimbo saba muhimu, huku uchunguzi wa maoni ukiashiria mashaka juu ya matokeo.

Harris anaelelekeza nguvu kwenye mji muhimu wa East Lansing, katikati mwa mashaka kutoka kwa Wamarekani wenye asili ya Kiarabu wanaochukizwa na msimamo wake kuhusu vita vya Gaza. 

Soma pia:Wagombea urais Marekani wapiga kampeni za lala salama Nevada

Trump hivi karibuni alitembelea mji wa Dearborn, akiahidi kumaliza vita vya Mashariki ya Kati. Vituo vyake vya kampeni vinahusisha Lititz, Pennsylvania, Kinston, North Carolina, Macon, na Georgia, akilenga wapigakura wa vijijini.

Katika siku zao za mwisho wa kampeni, Harris anasisitiza kupunguza gharama za maisha na kukosoa siasa za mgawanyiko za Trump. Trump kwa upande wake anamlaumu Harris kwa mfumuko wa bei na masuala ya uhamiaji.  Huku takribani watu milioni 75 wakiwa tayari wamepiga kura mapema, matokeo huenda yakachukuwa siku kadhaa kukamilishwa, hasa katika majimbo kama Pennsy-lvania.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW