1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Harris hatokutana na Putin iwapo Ukraine haitowakilishwa

8 Oktoba 2024

Kamala Harris amesema katika mahojiano na kituo cha habari cha CBS kuwa iwapo atachaguliwa kuwa rais hatokutana na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo ya amani ikiwa Ukraine haitawakilishwa.

Marekani | Kamala Harris
Makamu wa rais wa Marekani ambaye pia ni mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic Kamala HarrisPicha: Carolyn Kaster/AP Photo/picture alliance

Makamu wa rais wa Marekani ambaye pia ni mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic Kamala Harris amesema katika mahojiano kuwa, iwapo atachaguliwa kuwa rais hatokutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo ya amani ikiwa Ukraine haitawakilishwa.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha Habari cha CBS, Kamala Harris amesema Ukraine lazima iwe na sauti kuhusu mustakabali wake.

Soma pia: Zelensky: Umakini wa Marekani utaharakisha mwisho wa vita 

Awali, utawala wa Rais Joe Biden ulikataa kufanya mazungumzo yoyote na Putin.

Harris pia amekosoa sera za mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump juu ya Ukraine, akizitaja kama "kujisalimisha” kwa uvamizi wa Urusi.

Trump amekuwa akikosoa msaada mkubwa wa kijeshi na kifedha unaotolewa na Marekani kwa ajili ya Ukraine na kusisitiza kuwa na uwezo wa kufikia haraka makubaliano ya amani na Putin.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW