1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris, Walz wajitokeza kwa mara ya kwanza huko Philadelphia

Sylvia Mwehozi
7 Agosti 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amejitokeza kwa mara ya kwanza jukwaani akiwa na mgombea mwenza Tim Walz mjini Philadelphia. Walz alianza kwa kumshambulia Trump.

Harris na Walz
Kamala Harris na Tim WalzPicha: Joe Lamberti/AP/dpa/picture alliance

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amejitokeza kwa mara ya kwanza jukwaani akiwa na mgombea mwenza Tim Walz mjini Philadelphia. Walz, ambaye ni gavana wa Minnesota aliteuliwa jana na Harris kuwamgombea wake mwenza wa chama cha Democratic, katika uchaguzi wa Novemba.

Mara baada ya kupanda jukwaani, gavana huyo alitoa shutuma nzito dhidi ya mpinzani wao wa chama cha Republican Donald Trump, akihoji kujitolea kwake kwa taifa hilo na rekodi yake ya uongozi. Aidha, amemshambulia Trump kwa kudhoofisha uchumi, kudharau sheria na kuchochea machafuko na mgawanyiko.

Walz anajiunga na Harris ambaye sasa ndiye mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, katika mojawapo ya vipindi vigumu zaidi katika siasa za  za Marekani na kuweka mazingira ya kuwepo na kampeni kali na zisizotabirika za uchaguzi wa rais.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW