1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harry Kane: Hatuiogopi Real Madrid

19 Machi 2026

Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane amesema hawaiogopi kamwe Real Madrid.

Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane akisherehekea kufunga bao
Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane akisherehekea kufunga baoPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Hii ni baada ya Bayern kujikatia tiketi ya robo fainali ya Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya kufuatia ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Atalanta ya Italia usiku wa kuamkia Alhamis ambapo Kane alitia kimyani mabao mawili.

Baada ya ushindi huo Bayern sasa watakabiliana na Madrid huku Barcelona wakivaana na wapinzani wao kutoka Uhispania Atletico Madrid ambao licha ya kushindwa 3-2 na Tottenham Hotspur usiku wa jana, walifuzu.

Mabingwa watetezi Paris Saint Germain watapambana na Liverpool kisha Sporting Lisbon wa Ureno wakabiliane na Arsenal katika robo fainali ya mwisho.

Mkondo wa kwanza wa mechi hizo utakuwa Jumanne na Jumatano, Aprili 7 na 8.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW