Hasimu mkubwa wa Erdogan, Sheikh Gulen afariki dunia
21 Oktoba 2024Matangazo
Vyombo kadhaa vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa Sheikh Fethullah Gulen mwenye makaazi yake nchini Marekani amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini. Gulen alikuwa mhubiri ambaye serikali ya Uturuki ilimtuhumu kupanga jaribio la mapinduzi yaliyoshindikana mnamo mwaka 2016. Gulen alikuwa anaishi kwenye jimbo la Pennsylvania nchini Marekani tangu mwaka 1999. Alikuwa na umri wa miaka 83.
Tovuti ya Herkul, ambayo huchapisha mahubiri ya Gulen, imesema Sheikh Fethullah Gulen alifariki jana jioni baada ya kutibiwa ugonjwa wa muda mrefu.