1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hasira zaongezeka Kenya kuhusiana na utekaji wa wakosoaji

28 Desemba 2024

Watumiaji wanne wa mitandao ya kijamii walitoweka baada ya kuchapisha picha zilizotengenezwa na AI za Rais William Ruto ambazo zilionekana kuwa za kuudhi kwa wafuasi wa serikali.

Kenya Nairobi 2024 | Polisi kuingilia kati maandamano dhidi ya kanuni mpya za ushuru
Polisi Kenya wanatahumiwa kuhusika na matukio ya kutoweka kwa wakosoaji wa utawala wa Rais Ruto, tuhuma ambazo wanakanusha.Picha: Gerald Anderson/Anadolu/picture alliance

Makundi ya haki za binadamu, wanasheria, na wanasiasa nchini Kenya wameeleza wasiwasi kuhusu wimbi jipya la utekaji wa wakosoaji wa serikali, hasa vijana ambao wamemkosoa Rais William Ruto mtandaoni.

Polisi imekana kuhusika na utekaji huo, lakini inakosolewa kwa kushindwa kuchunguza matukio hayo. Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu iliripoti visa 82 vya utekaji nyara tangu Juni, na watu 29 bado hawajulikani walipo.

Soma pia: Mamlaka Kenya zakanusha kuwateka wakosoaji wa serikali

Chama cha Wanasheria cha Kenya, LSK, na mashirika mengine yanataka hatua za haraka dhidi ya watekaji au mkuu wa polisi kujiuzulu.

Naibu wa Rais alieondolewa Rigathi Gachagua, baada ya kutofautiana na Ruto kuhusu maandamano ya vijana, amedai kuwepo na kikosi cha siri kinachohusika na utekaji. Mahakama ya Kenya imeonya kuwa utekaji nyara ni tishio kwa haki za raia na imeitaka serikali kufuata sheria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW