Hatima ya Pistorius kujulikana Septemba 11
12 Agosti 2014Hiyo ni wakati wakili huyo akichukua hatua ya mwisho kumuokoa mwanariadha huyo dhidi ya kifungo cha maisha.
Katika maelezo yake wakati wa akifunga hoja yake , wakili huyo Barry Roux amejaribu kuvunja madai ya upande wa mashtaka kuwa mteja wake alimuua kwa makusudi Reeva Steenkamp aliyekuwa na umri wa miaka 29 baada ya kutokea kutokuelewana alfajiri ya siku ya wapendanao mwaka 2013.
Ushahidi wa mwisho umeelezea upande usiofahamika kabisa wa Oscar, mwenye umri wa miaka 27, kwamba alimpiga Reeva risasi nne akiwa kwenye bafu akiwa hasa na dhamira ya kumuua. Kwa mujibu wa waendesha mashitaka, Oscar ni "mdanganyifu" mwenye kipaji cha kudanganya. Jaji Thokozile Masipa atatoa hukumu ya kesi hiyo tarehe 11 mwezi Septemba.
Mwandishi: Sekione Kitojo/AFP
Mhariri: Josephat Charo