Hatimaye Soka: Mabingwa wa Ujerumani waanza ligi kwa kishindo.
6 Agosti 2005Matangazo
Mabingwa wa ligi ya soka ya Ujerumani Bundesliga, Bayern Munich wameanza msimu huu kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 3 – 0 dhidi ya Borussia Monchengladbach.
Bayern ilianza kulifumania lango la Borussia katika dakika ya 28 kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Owen Hargreaves.
Mshambuliaji wa kiamtaifa wa Uholanzi Roy Makaay alifunga kitabu cha magoli kwa kupachika mabao mawili kwa Bayern katika dakika nne za mwisho.