UchumiAfrika
Hatma ya mkataba wa AGOA bado kitendawili
30 Septemba 2025
Matangazo
Mkataba wa kibiashara wa AGOA, unaotoa fursa ya kusaidia ukuaji barani Afrika, unafikia tamati leo Jumanne huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu iwapo Marekani itaurefusha.
Kumalizika kwa mkataba huo kunahatarisha maelfu ya ajira barani Afrika, ikiwemo nchini Kenya ambako AGOA imeimarisha sekta ya utengenezaji wa vitambaa na mavazi, na kuiwezesha kushindana na wazalishaji kutoka mataifa ya Asia kama Bangladesh na Vietnam.
Utawala wa Rais Donald Trump umesema unaunga mkono kurefusha mkataba huo kwa mwaka mmoja. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, AGOA imefanikisha maelfu ya bidhaa kutoka mataifa ya Afrika yaliyokidhi vigezo kuuzwa katika masoko ya Marekani bila ushuru.