1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usajili wa maeneo ya Palestina wakosolewa

16 Februari 2026

Hatua ya serikali ya Israel kuidhinisha mchakato wa kusajili ardhi kwenye Ukingo wa Magharibi imelaumiwa na mataifa ya Kiarabu na wakosoaji waliouita "unyakuzi mkubwa wa ardhi".

Maeneo ya Wapalestina Nablus 2026 | Wapalestina wakipita kwenye uzio uliopambwa kwa bendera za Israel zilizowekwa na walowezi katika kituo cha treni
Hatua ya Israel ya kuidhinisha usajili wa ardhi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi imekosolewa na mataifa ya KiarabuPicha: Jaafar Ashtiyeh/AFP

Hatua ya serikali ya Israel kuidhinisha mchakato wa kusajili ardhi kwenye Ukingo wa Magharibi, imelaumiwa na mataifa ya Kiarabu na wakosoaji waliouita "unyakuzi mkubwa wa ardhi" ambao ungeharakisha pia unyakuzi wa ardhi hiyo ya Palestina.

Misri, Qatar na Jordan wamekosoa hatua hiyo wakiitaja kuwa haramu na inayokiuka sheria ya kimataifa.

Kwenye taarifa yao, Misri imesema uamuzi huo ni hatari na unaolenga kudhibiti maeneo yanayokaliwa na Kipalestina, huku Qatar ikisema ni uamuzi unaolenga kuibadilisha ardhi ya Ukingo wa Magharibi kuwa mali ya serikali, na ambao utawanyima Wapalestina haki zao.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilisema ni hatua ambayo ingewezesha "ufafanuzi wa wazi na wa kina wa haki za kutatua migogoro" na ilihitajika kufuatia usajili haramu wa ardhi katika maeneo yanayodhibitiwa na Mamlaka ya Palestina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW