Jeshi na waasi wakabiliana nchini Mali
2 Oktoba 2023Matangazo
Kuongezeka kwa ghasia kunaendana na hatua inayoendelea ya kuondolewa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kufanikisa amani nchini humo.
Kwa upande wake jeshi la Mali limesema jana Jumapili limekiri kuhusika katika vita na waasi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa nchi hiyo.
Ripoti ya jeshi katika mitandao ya kijamii ilisema kumekuwa na 'mapigano makali' dhidi ya 'magaidi' katika eneo la Bamba ambalo waasi wanaotaka kujitenga wanadai kulidhibiti.
Kambi ya kijeshi ya Bamba huko Gao ni ya nne kuchukuliwa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyotekelezwa tangu Agosti na waasi wa kundi la harakati za Azawad.
Mashambulizi hayo yalifuatia kuondoka kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao ulisaidia kudumisha hali ya utulivu kwa miaka mingi.