1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatua za kuzingatia unapojihisi umeambukizwa Ebola

Kriesch, Adrian5 Desemba 2014

Taasisi ya Matibabu ya Robert Koch nchini Ujerumani inapendekeza muongozo na hatua za kwanza katika kuchunguza na kubainisha dalili za ugonjwa wa Ebola.

Schulen in Liberia öffnen wieder Monrovia 2015
Picha: DW/J. Kanubah

Taasisi ya Matibabu ya Robert Koch nchini Ujerumani inapendekeza muongozo na hatua za kwanza katika kuchunguza na kubainisha dalili za ugonjwa wa Ebola:

Mgonjwa anapoonyesha dalili za homa (yaani kiwango cha joto mwilini kinachozidi nyuzi 38.5°C), kuharisha, kichefuchefu, na kutapika.

Ili kuambukizwa, ni lazima mtu awe amepitia mojawapo ya njia zifuatazo:

  • Awe ametangamana na mtu anayeugua ugonjwa wa Eobla, amegusana kimwili na muathirika wa virusi vya Ebola, au mtu aliyefariki kutokana na Ebola ndani ya kipindi cha siku 21 baada ya dalili za kwanza za ugonjwa huo kuonekana.

AU

  • Awe amefanya kazi katika maabara, hospitali, au katika mazingira ambako huenda alitangamana na watu walioambukizwa virusi, au kushika damu na majimaji ya mwili kutoka kwa waathiriwa ndani ya muda wa siku 21 baada ya dalili za ugonjwa huo kuonekana.

AU

  • Ameishi au kuzuru mataifa yanayokumbwa na tisho la ugonjwa huu wa Ebola kama vile Liberia, Sierra Leone, Guinea, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndani ya muda wa siku 21 baada ya kupatikana na dalili hizi.

AU

  • Amekula nyama au kuwashika wanyamapori mfano popo, kima na tumbili.
Laini ya simu ya dharura mjini Lagos, NigeriaPicha: DW/A. Kriesch

Endapo hatua hizi zote zitathibitishwa, basi mtu anahitajika kumuona daktari upesi au kutoa habari kwa afisa wa afya katika eneo husika. Laini za simu ya dharura kuhusu ugonjwa wa Ebola zimefunguliwa hasa katika maeneo ambako ugonjwa huu umezuka. Mtu anapopiga simu kwa kutumia nambari hizi za dharura wahudumu hutoa ushauri kuhusu ni wapi na jinsi gani mtu anavyoweza kuhudumiwa. Pia ni muhimu kutoa maelezo sahihi kuhusu afya yako kwa mafisa wa matibabu. Kumbuka una nafasi nzuri ya kutibiwa na kupona ugonjwa huu endapo utagunduliwa mapema.

Baada ya kupatikana na virusi vya Ebola, mgonjwa anapasa kujitenga kabisa na wengine, mfano asisalimiane kwa mikono, kumbusu mwengine, au kufanya tendo la ngono

Sampuli za damu, mate na mkojo lazima zipelekwe maabara yenye vifaa vya kuaminika ili kufanyiwa uchunguzi wa kina kubainisha mapema virusi vya Ebola.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi