1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatua za Trump zaendelea kuibua hisia mseto Davos

23 Januari 2025

Kongamano la Kimataifa la Uchumi linaendelea mjini Davos, nchini Uswisi, huku likiwa limegubikwa na kiwingu cha kurejea kwa Rais Donald Trump wa Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa ofisini mwake katika ikulu ya White House mnamo Januari 20, 2025
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Carlos Barria/REUTERS

Hata wakati ambapo Donald Trump hakuwepo katika vyumba vya mkutano huo wa kimataifa, au hata kuwa mada kuu, ameendelea kuibua gumzo miongoni mwa washiriki wa mkutano huo siku ya Jumatano.

Hisia zaidi ziliendelea kutolewa kuhusu matamshi na vitisho vya Trump.

Mfereji wa Panama sio zawadi kutoka Marekani

Katika kikao kimoja, Rais wa Panama Jose Raul Mulino alisema kwamba Mfereji wa taifa hilo haukuwa zawadi kutoka kwa Marekani baada ya Trump kusema kuwa ataumiliki tena.

Guterres amsifu Trump

Ingawa baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa wana wasiwasi kuhusu rais huyo mpya wa Marekani, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alimsifu Trump kwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza.

Guterres amesema kulikuwa na mchango mkubwa wa diplomasia imara kutoka kwa Trump ambaye wakati huo alikuwa bado rais mteule wa Marekani.

Gumzo la ushirikiano na Trump latawala Jukwaa la Uchumi Duniani

Wakati huo huo, Rais wa Argentina Javier Milei anayemshabikia zaidi Trump, alisema kwamba ulimwengu unapaswa kusherehekea kurejea madarakani kwa Rais Trump, na kuongeza kuwa enzi ya dhahabu anayopendekeza kwa Marekani itaangazia dunia nzima.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio GuterresPicha: Pedro Nunes/REUTERS

Katika mahojiano na Boomerang huko Davos, Rais Milei alisema anajitahidi kupata mkataba wa biashara huria na Marekani.

Shinikizo laongezeka dhidi ya sekta za kibinafsi

Shinikizo linaloongezeka la Rais Trump kwa sekta ya kibinafsi kuachana na programu mbalimbali, zimewaacha baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa Davoswakitafuta maneno mapya ya kuelezea taratibu zao za kikazi ambazo ni muhimu kwa biashara zao.

Trump akatiza mipango mbali mbali

Trump ametoa mfululizo wa amri za kukatiza mipango mbalimbali ya serikali yake ya usawa na ushirikishwaji (DEI), ambayo inajaribu kukuza fursa kwa wanawake, jamii za walio wachache na makundi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, pamoja na makundi mengine ambayo kwa kawaida yanakosa uwakilishaji.

UN yatoa wito kwa mataifa kuongeza juhudi za kulinda mazingira

Hatua za Trump juu ya mipango hiyo ya DEI, zimejadiliwa katika vyumba vya mkutano huo wa Davos ambapo usawa wa kijinsia, nguvu kazi mbalimbali na uwakilishi bora wa walio wachache duniani kote vinaendelea kuwa malengo muhimu.

Serikali mpya ya Syria kufanya kazi na makundi yote ya watu

Waziri wa mambo ya nje wa Syria Asaad al-Shaibani amesema serikali mpya ya nchi hiyo itaendelea kufanya kazi kwa kujumuisha makundi yote ya watu.

Wakati wa mazungumzo na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair huko Davos, al-Shaibani alisema kuwa hakuna mtu anayepaswa kuadhibiwa kwasababu ya asili yake, au misingi ya kijamii na kidini ama pia ushirikiano na makundi fulani.

Waziri huyo alitoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa utulivu wa nchi hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW