1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatutamtegemea Trump ili kubadili mazingira

Jane Nyingi
10 Novemba 2016

Mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi COP 22 umeingia siku yake ya nne mjini Marrakeshi nchini Morocco, huku washiriki wakitoa ujumbe kwa Trump

Marokko Marrakesch Weltklimakonferenz UN Climate Change Conference COP22
Picha: picture-alliance/dpa/M. Messara

Washiriki wamesema hawatomkubalia rais mteule wa Marekani Donald Trump ambae ameonekana kutounga mkono makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kuvuruga mchakato wa ulimwengu  kuondokana na nishati chafu. Washiriiki hao wamesema iwapo  atachukua msimamo wasiokubaliana nao basi Marekani itasalia kivyake nyuma katika hilo..Huku kukiwa na hofu kuwa  rais mteule  Donald Trump  huenda akazingatia  ahadi aliyotoa wakati wa kampeini zake ya kuiondoa Marekani katika mapatano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, Australia  imekuwa nchi ya hivi punde kutia saini mapatano hayo. Mapatano hayo yanalenga kukabiliana na kupanda kwa joto duniani.

Kiwanda cha kemikali MarekaniPicha: Reuters

Tofauti na rais Barrack Obama  ambae aliyafanya mabadiliko ya tabia nchi  kuwa miongoni mwa sera muhimu katika utawala wake,Trump mara kwa mara katika mitandao ya kijamii amesema kupanda kwa joto duniani ni mzaha na hakubaliani na hilo.Washiriki katika mkutano wa Morocco walikuwa na hilli la kumweleza Trump “Makubaliano ya Paris hayatamtegemea  hatua ya Donald Trump, kukataa kukubali  mabadiliko ya tabia nchi. Makubaliano ya Paris yatategemea uwezo wa vijana na watu wengine ulimwenguni  kote  kuchukua  hatua” Marekani  ndio ya pili duniani katika uchafuzi wa mazingira  baada ya China, ikitoa asilimia 13 ya gesi chafu.

Tayari zaidi ya mataifa 100 yanayowakilisha asilimia 70 ya gesi chafu zinazozalishwa duniani yametia saini mapatano hayo ya kihistoria, yaliyoanza kutekelezwa mapema  mwezi huu. Uchaguzi wa kitaifa uliofanyika nchini Australia mwezi Julai mwaka huu ndio uliochelewesha maafisa wake kutia saini mapatano hayo.Hatua hiyo itaisadia Australia kupunguza uzalishaji hewa chafu kwa kati ya asilimia 26-28 kufikia mwaka 2030. Pamoja na matumizi  makubwa ya nishati inayotegemea makaa ya mawe na idadi ndogo ya  watu  millioni 22, Australia  inachukuliwa kuwa mojawapo ya  wachafuzi  wakubwa wa mazingira duniani. Nayo serikali ya Ujerumani  katika siku kadhaa zijazo inakamilisha  utayarishaji maelezo yake yanayopaswa kuwasilishwa katika mkutano huo wa 22 wa tabia nchi unaofanyika nchini Morocco.

Waziri Sigmar GabrielPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Waziri wa uchumi Sigmar Gabriel  ambae ni kiongozi wa chama cha Social Democrat SDP chama kinachogawana madaraka na kile cha Conservative chake kansela Angela Maerkel  amesema Ujerumani  imedhamiria kupunguza kwa asilimia 50 utoaji wa gesi za sumu kutoka viwandani zinazoongeza kiwango cha joto duniani ifikiapo mwaka 2050. Kufikia mwaka 2030 waziri huyo amesema  utoaji huo wa gesi chafu utakuwa umepunguzwa kwa asilimia 55

Mwandishi: Jane Nyingi/RTRE/AFPE
Mhariri: Iddi Ssessanga

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW