1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA : Sudan haitaki vikosi vya Umoja wa Mataifa Dafur

17 Septemba 2006

Rais Omar al- Bashir wa Sudan kwa mara nyegine tena amesema hataki kuwekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Dafur chini ya mazingira yoyote yale.

Bashir alitowa kauli hiyo baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na upande wowote mjini Havana Cuba.Amesema katika mazungumzo yake hayo wameyakinisha kwa ufasaha kwamba wanapinga uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutuma wanajeshi Dafur.

Bashir amesema Sudan imeanzisha uhusiano wa karibu na Pakistan,India,China na Malaysia na iko katika nafasi ya kuhimili vikwazo vyovyote vile dhidi yake.Pia ameipongeza Cuba kwa kuendelea kuishi zaidi ya miaka 40 ikiwa chini ya vikwazo vya Marekani.

Kwa upande wake Annan ameihimiza serikali ya Sudan kukubali uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutuma wanajeshi 20,000 wa kimataifa wa kulinda amani kuchukuwa nafasi ya wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika walioko Dafur hivi sasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW