HAVANA : Wapinzani wa Cuba wakutana Havana
22 Mei 2005Matangazo
Makundi ya upinzani yamekusanyika hadharani nchini Cuba kwa mkutano wa hadhara wa siku mbili karibu na mji mkuu wa Havana.
Zaidi ya watu 200 wamehudhuria mkutano huo mkuu ulioandaliwa na Baraza la Kuendeleza Vyama vya Kijamii. Wamekuwa wakidai kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa nchini humo na kukomesha mfumo wa utawala wa chama kimoja. Maandamano ya hadhara ya upinzani ni jambo la nadra nchini Cuba lakini waandishi wanasema kumekuwa hakuna jaribio la moja kwa moja la serikali kuzuwiya mkutano huo.
Hata hivyo serikali imewatimuwa wanasiasa kadhaa wa Ulaya ambao walipanga kuhudhuria mkutano huo ikiwa ni pamoja na mbunge wa Ujerumani wa chama cha Christian Demokrat Arnold Vaatz na mbunge wa Czech Karel Schwarzenberg.