Havana.mkutano wa 14 wa umoja wa NAM kufanvika Cuba.
12 Septemba 2006Matangazo
Waziri wa masuala ya kigeni wa Cuba Felipe Perez Roque amefungua mkutano wa kumi na nne wa maendeleo wa nchi zisisofungamana na upande wowote mjini Havana.
Amewataka washiriki waweke kando khitilafu zao na kuzidi kushirikiana zaidi.
Aidha amelaumu vita vilivyopita kati ya Israel na Lebanon na kuviita kuwa ni mauaji ya kila siku ya raia wa Palestina.
Rais wa Iran Mahmud Ahmadinejad anategemewa kuhudhuria mkutano huo, pamoja na rais wa Pakistan Perves Musharraf, waziri mkuu wa India Manmohan Singh, rais wa Venezuela Hugo Chavez na rais wa Syria Bashar el- Assad.
Cuba ndio mwenyekiti wa sasa wa muoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote ikikabidhiwa wadhifa wa miaka mitatu uliokamilishwa na Malaysia.