1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hegseth: Marekani inapigana kushinda katika mzozo wa Iran

2 Machi 2026

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amezungumzia wasiwasi unaoongezeka kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel nchini Iran yanaweza kugeuka kuwa mzozo wa kikanda wa muda mrefu, akisema hiyo sio Iraq.

Brüssel 2025 | Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth katika mkutano na kundi la nchi washirika wa Ukraine
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth Picha: Yves Herman/REUTERS

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amezungumzia wasiwasi unaoongezeka kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel nchini Iran yanaweza kugeuka kuwa mzozo wa kikanda wa muda mrefu, akisema hiyo sio Iraq.

Hegseth, alikuwa akizungumza kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari, tangu mashambulizi ya Jumamosi, akiambatana na mkuu wa jeshi la anga, Dan Caine. Alipoulizwa ikiwa kwa hivi sasa, Marekani inao wanajeshi wake katika ardhi ya Iran, ameeleza kuwa;

"Hapana! lakini hatutaingia katika maelezo ya kile tutakachofanya au tusichofanya. Nadhani ni mojawapo ya makosa ambayo kwa muda mrefu idara hii au marais au wengine wanapaswa kuwaelza Wamarekani na maadui zetu, kwamba hiki ndicho tutafanya. Na kwa hivyo Rais Trump anahakikisha kwamba maadui zetu wanaelewa kwamba tutafika mbali kadri tunavyohitaji ili kuendeleza maslahi ya Marekani."

Waziri huyo amesema operesheni hiyo ya Marekani ilikuwa na dhamira ya wazi ya kuondoa kitisho cha makombora ya Iran, kuharibu jeshi lake la wanamaji na kutokuwepo kabisa silaha za nyuklia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW