1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heiko Maas amaliza ziara yake Afrika

1 Machi 2019

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Heiko Maas, amemaliza ziara yake ya Afrika Magharibi, ambayo kituo chake cha mwisho kilikua nchini Mali.

Bundesaußenminister Heiko Maas in einem Airbus A 340
Picha: picture-alliance/dpa/R. Hirschberger

Tarehe 28 Februari ilibidi arudi Ujerumani, lakini ndege yake iliharibika hivyo kupelekea abaki Bamako mpaka kesho yake hili kurudi Ujerumani kwa ndege nyingine. 

Safari hiyo ya Mali, ilikuja siku nne baada ya magaidi kushambulia kambi ya mafunzo ya Umoja wa Ulaya nchini humo.

Maas aliwatembelelea wanajeshi wa Ujerumani wapatao 800 katika kambi hiyo. Ni walinzi watatu wa Mali walioumizwa.

Hamna mwanajeshi kutoka Ujerumani aliyeumizwa. Mpaka sasa inasadikiwa kwamba shambulio hilo lilifanywa na magaidi wawili waliofanya shambulio la kujitoa mwanga.

Picha: Imago/X. Heinl

Waziri huyo wa Mambo ya nje alienda Mali kutembelea wanajeshi wa Ujerumani wapatao 800 ambao wapo huko wakisaidia kuimarisha amani nchini humo na kufundisha wanajeshi wa Mali kudhibiti ugaidi.

Heiko Maas aliwaomba wanajeshi hao waendelee kukaa kambini hapo na kusema kwamba itakua ni jambo baya kama Ujerumani ikiondoka nchini humo. Kitendo hicho kitapelekea magaidi kujipanga upya na kupelekea jitihada zote zilizofanyika mpaka sasa kuwa ni bure.

Tatizo la Ugaidi Mali

Kusini mwa Mali kuliingia kwenye mikono ya waasi mwaka 2012. Waasi hao walitaka uhuru wa eneo hilo na kutaka kuanzisha dola la kiislam. Januari 2013, walitishia kuvamia mji mkuu wa Mali, Bamako.

Picha: Getty Images/A. Koerner

Hiyo ilipelekea majeshi ya Ufaransa kulisaidia jeshi la Mali kukomboa eneo hilo lililoangukia kwenye mikono ya waasi. Baadaye Julai 2013, vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa navyo viliingia Mali kusaidia kupelekea usitishwaji wa mapigano na kuingiwa kwa makubaliano ya amani. 

Carina Böttcher mtaalam wa maswala ya amani ya kimataifa anaamini kwamba Mali ni kati ya sehemu hatari duniani ambapo majeshi ya Ujerumani yapo. Akaongeza kuwa mashambulizi kama hayo yaliyotokea kwenye kambi ya mafunzo yataendelea kutokea.

Kwa Ujerumani na kwa umoja wa Ulaya, amani nchini Mali ni jambo muhimu sana katika sera zao za mambo ya nje. Böttcher anaamini kwamba ugaidi unaoendelea nchini Mali utapelekea watu wengi kukimbia na kuelekea Ulaya.

Kwahiyo juhudi kubwa zinafanyika kuweza kuhakikisha amani inakuepo katika eneo hilo.

Mhandishi: Harrison Mwilima/DW News

Mhariri: Saum Mwasimba