Helikopta ya Rwanda yadunguliwa DR Congo
7 Aprili 2026
Msemaji wa jeshi la FARDC kwenye operesheni za kijeshi kwa jina ma Sokola 2 katika jimbo la kivu kusini, Luteni Reagan Mbuyi amesema ndege iliyoangushwa ilitokea Rwanda na kuwa walifanikiwa kuwafukuza waasi wa Twirwaneho huku wengine wakijisalimishwa.
"Moja ya helikopta hizo kutoka Rwanda, tuliitungua helikopta hiyo na kufuatia operesheni hiyo, kulikuwa na wapiganaji wa waasi 13 wa kundi la Tugwaného na M23 AFC waliojisalimisha kwa FARDC. Mapambano yanaendelea vyema na kituo mji wa Minembwe ni mali yetu. Kusini na kaskazini tayari zimebitiwa na usalama umeimarishwa vizuri. Leo hii tarafa ya Uvira, hata ile ya Fizi, ziko nje ya hatari."
Aidha Luteni Reagan ameongeza kuwa hali imerejea kuwa shwari na kwamba jeshi limerejesha udhibiti wa kijiji cha Muramvya, katika kundi la Bijombo.
"Hali ya leo, kuna utulivu katika eneo hili, kote upande wa tarafa ya Fizi na upande wa tarafa ya Uvira. Tumekamata tena miji ya Mitamba na Muramvya. Kwa hivyo, ili kuelewa vizuri, Muramvya tayari inatupa njia ya kufikia kijiji cha Muketi ambacho kinakuongoza kuelekea Bijombo, ili kudhibiti wilaya zetu zote jirani kwa madhumuni ya kufunga kila njia kwa adui."
Licha ya jeshi kusema kuwa hali imekuwa shwari, vyanzo vya ndani kwenye eneo la vita vimesema, mapigano yalianza tena hii leo saa kumi na moja na dakika arobaini na tano alfajiri huko Mikenge na katika maeneo jirani. Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linapambana na waasi wa Twighaneho na Red_Ntabara, washirika wa waasi wa M23_AFC.
Mashuhuda wamesema kulikuwa na majibizano makali ya risasi, hali iliyowatumbukiza wakazi katika hofu na wasiwasi.