1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah, Israel zashambuliana vikali usiku kucha

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah zimeshambuliana vikali usiku wa kuamkia leo Jumapili, huku ndege za kivita za Israel zikifanya mashambulizi makali zaidi katika eneo la kusini mwa Lebanon.

Mlipuko mjini Beirut
Magari yaliyoharibiwa katika eneo la shambulizi la Ijumaa la Israeli katika vitongoji vya kusini mwa BeirutPicha: Bilal Hussein/AP/picture alliance

Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah zimeshambuliana vikali usiku wa kuamkia leo Jumapili, huku ndege za kivita za Israel zikifanya mashambulizi makali zaidi katika eneo la kusini mwa Lebanon na Hezbollah kurusha makombora kuelekea kaskazini mwa Israel. Hofu ya mzozo wa Mashariki ya Kati kusambaa bado yatawala

Jeshi la Israel limedai kuyalenga maeneo takribani 290 jana Jumamosi, ikiwemo maelfu ya mapipa ya kurusha makombora ya Hezbollah na kuapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na serikali ya Iran. Kwa upande wake, Hezbollah nayo imedai kuilenga kambi ya anga ya Ramat David ya Israel kwa makombora chungu nzima  kujibu mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel dhidi ya Lebanon.

Mashambulizi hayo yanayozidi kuongezeka yamefanyika chini ya saa 48 baada ya shambulizi la anga la Israel lililowalenga makamanda wa Hezbollah katika kitongoji kimoja mjini Beirut na kuwaua watu 45.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW