1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Hezbollah yapambana na wanajeshi wa Israel, Lebanon

18 Novemba 2024

Wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon, wamesema vikosi vyao vimerusha makombora manne kuwalenga wanajeshi wa Israel katika mji wa Khiam siku ya Jumatatu.

Lebanon | Mlipuko, Beirut
Mashambulizi kati ya Lebanon na Israel yamesababisha maafa makubwa ya kibiaanadamuPicha: Mohammed Yassin/REUTERS

Hapo jana Jumapili, wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran pia waliripoti kufanya mashambulizi saba dhidi ya vikosi vya Israel katika eneo hilo hilo.

Vyombo vya Habari nchini Lebanon vimeripoti kwamba jeshi la Israel limeanza upya mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya wanamgambo hao.

Vita vya Lebanon vinavyoendelea wakati saw ana vita vya Gaza, vimesababisha hali ya kibinadamu nchini Lebanon kuwa mbaya zaidi.

Kulingana na takwimu rasmi za wizara ya afya ya Lebanon, zaidi ya watu 3, 400 wameuawa na 14,700 wamejeruhiwa.

Wizara hiyo haitofautishi vifo vya rai ana vile vya wanamgambo wa Hezbollah.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW