Hezbollah yakataa mpango wa usitishaji mapigano
4 Juni 2026
Hezbollah imekataa mpango wa kusitisha mapigano uliokubaliwa na Lebanon na Israel katika mazungumzo yaliyosimamiwa na Marekani. Israel inaendelea na mashambulizi kusini mwa Lebanon na imesisitiza haitajiondoa katika eneo hilo.
Marekani imesema makubaliano hayo yangetegemea Hezbollah kusitisha mashambulizi na kuondoa wapiganaji wake karibu na mpaka. Lakini kiongozi wa Hezbollah, Naim Qassem, ameitaja hatua hiyo kuwa "ramani ya kuwaangamiza Walebanon,” akisisitiza kuwa mapambano yataendelea kwa muda wote ambao Israel itaendelea kuwepo katika maeneo yanayokaliwa.
Aidha Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema Israel itaendelea na mashambulizi yake nchini Lebanon kwa sasa. Israel pia imesema haitaondoa majeshi yake kusini mwa Lebanon, huku jeshi lake likiendelea kushambulia maeneo inayodai kutumiwa na Hezbollah.