1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah yakiri Israel kumuua kamanda wake mwingine

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Kundi la Hezbollah limethibitisha hii leo kifo cha afisa wake wa ngazi ya juu Nabil Kaouk kutokana na shambulizi la Israel.

Mashambulizi ya Israel dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon
Mashambulizi ya Israel dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon.Picha: Jim Urquhart/REUTERS

Mauaji hayo yametokea siku moja baada ya kundi hilo la Lebanon kukiri kuuawa kwa makamanda wake kadhaa, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Hassan Nasrallah.

Taarifa hiyo imekuja saa kadhaa baada ya shambulio la ndege la Israel, kaskazini-mashariki mwa Lebanon kuwaua watu 11. Israel imesema zaidi ya wanachama 20 wa Hezbollah waliuawa pamoja na Nasrallah.

Umoja wa Mataifa unasema idadi ya watu waliohamishwa na mzozo huo kutoka kusini mwa Lebanon imeongezeka zaidi ya maradufu na sasa inasimama kwa zaidi ya 211,000.

Wakati huo huo, vyanzo viwili vya habari vimesema shambulizi la Israel limemuua mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la Kisunni la Jama'a Islamiya Mohammad Dahrouj.

Kundi hilo limeripotiwa kufanya mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel mwaka uliopita, na Israel imefanya mashambulizi yaliowalenga viongozi wengine waandamizi wa kundi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW