1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah yamtangaza Naim Qassem kuwa kiongozi mpya

29 Oktoba 2024

Kundi la Hezbollah limemtangaza Naibu Mkuu Naim Qassem kuwa kiongozi baada ya kuuliwa Hassan Nasrallah, katika shambulio la Israeli kusini mwa Beirut mwezi uliopita.

Naim Qassem | Hezbollah
Kiongozi mpya wa kundi la Hezbollah Naim QassemPicha: Houssam Shbaro/Anadolu/picture alliance

Baraza la uongozi la kundi hilo limesema limekubali kuchaguliwa Sheikh Naim Qassem, kuwa katibu mkuu wa Hezbollah.

Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran limesema limeazimia kuendelea na mapambano mpaka ushindi dhidi ya Israel upatikane, baada ya vita kuzuka mnamo mwezi Septemba.

Israel na Hezbollah zashambuliana kwenye maeneo muhimu

Sheikh Qassem mwenye umri wa miaka 71 ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa kundi hilo  lililoundwa mnamo mwaka 1982 na amekuwa naibu kiongozi wa kundi hilo tangu mwaka 1991.