1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah yavurumisha maroketi karibu na Tel Aviv

25 Novemba 2024

Mji wa Tel Aviv umeshambuliwa kwa roketi kadhaa na wapiganaji wa Hezbollah. Jeshi la Israel limesema katika tukio hilo la jana Jumapili, nyumba kadhaa zimebomolewa na nyingine ziliwaka moto karibu na mji huo wa Tel Aviv.

Bendera ya Kundi la Hezbollah la nchini Lebanon
Bendera ya Kundi la Hezbollah la nchini Lebanon.Picha: dpa/picture alliance

Mji wa Tel Aviv ulishambuliwa baada ya Israel kufanya shambulio kubwa la anga katika mji wa Beirut, ambako watu 29 waliuawa mwishoni mwa wiki.

Hezbollah imesema pia imeshambulia sehemu mbili za kijeshi mjini Tel Aviv na kwenye vitongoji vya mji huo kulipiza kisasi. 

Polisi nchini Israel imeeleza kuwa athari ya mashambulizi ya Hezbollah imeshuhudiwa katika eneo la Petah Tikvah, upande wa mashariki wa Tel Aviv na kwamba watu kadhaa wamepata majeraha madogo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW