Hichilema bado ana matumaini kupatikana wachimba madini 25
6 Desemba 2023Matangazo
Wachimbaji hao wamekwama baada ya kutokea kwa maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.
Mvua hizo ziliyafanya machimbo hayo kufurika katika maeneo manne tofauti ya migodi ya shaba.
Soma zaidi: Yellen azuru Zambia kujadilia madeni ya China, afya ya umma
Kulingana na serikali ya Zambia machimbo hayo ni ya mgodi wa Seseli yaliyo katika eneo la Chingola umbali wa kilomita 250 kaskazini mashariki mwa Lusaka.
Juhudi za uokoaji zinaendelea wakati timu za uokoaji wakiwemo wanajeshi na makampuni mengine makubwa yakichukua tahadhari kutokana na utelezi unaopunguza kasi ya operesheni hiyo