1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yashambulia maeneo ya Iran nchini Syria

9 Novemba 2023

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin amesema ndege za kivita za Marekani zimeshambulia ghala ya silaha iliyoko kwenye eneo linalohusishwa na Iran.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema Marekani iko tayari kupambana ili kuwalinda watu wake
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema Marekani iko tayari kupambana ili kuwalinda watu wakePicha: Getty Images

Eneo hilo liko mashariki mwa Syria na Marekani ililshambulia jana Jumatano, ikilipiza kisasi cha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wake.

Austin amesema kwenye taarifa yake kwamba wanajeshi wa Marekani walifanya shambulizi la kujilinda katika kambi yake, mashariki mwa Syria baada ya wanajeshi wake kushambuliwa nchini Iraq na Syria.

Amesema, Marekani imejiandaa kikamilifu kuchukua hatua zaidi za kuwalinda watu wake pamoja na kambi zao.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha wiki mbili kwa Marekani kulenga maeneo kama hayo nchini Syria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW