Hilary Clinton azuru Baghdad
29 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Baada ya ziara fupi ya Rais George W. Bush mjini Baghdad, naye Seneta wa Mkoa wa New York, Bibi Hilary Clinton amewazuru wanajeshi wa Kimarekani katika mji mkuu wa Iraq. Mke huyo wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alitoa mwito wa kufanyiwa marekibisho siasa ya mambo ya nje ya Marekani. Kufuatana na kutishwa hali ya usalama ya wanajeshi wa Kimarekani na kutokana na ugumu wa kukabidhiwa madaraka kwa Wairaq wenyewe, mgogoro huo lazima uwekwe katika udhamini wa kimataifa, alisema. Kwa hivi sasa Marekani itahitaji msaada wa UM, alisisitiza Bibi Clinton. - Upande wake, mshauri wa mambo ya usalama wa Marekani Bibi Condeleeza Rice alitangaza kwamba Marekani inazingatia uwezekano wa kufanywa uchaguzi wa mojakwa moja wa serikali ya mpito ya Iraq. Alisema Mtawala wa Mambo ya Kiraiya wa Kimarekani Paul Bremer analizungumza shauri hilo pamoja na viongozi wa Washiya wa Kiiraq. Leo aliuawa mwanajeshi mmoja wa Kimarekani kiliposhambuliwa kituo cha wanajeshi mjini Mossul huko Iraq ya Kaskazini.