Hillary Clinton awasifu waasi wa Libya
19 Oktoba 2011Mwanadiplomasia huyo alito ahadi kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kulisaida baraza la mpito la waasi wa Libya kurejea katika mkondo wa demokrasia.
Akizungumza na viongozi wa Baraza hilo mjini Tripoli; Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema kuwa Walibya waliupiga vita udikteta uliokuwako na wamefanikiwa kurejesha haki za taifa lililo huru.
Bibi Clinton alisisitiza kuwa Marekani itauunga mkono mfumo utakaoyapa kipa umbele masuala ya demokrasia na makundi yanayotaka kuivuruga mipango hiyo yatalazimika kupambana na Walibya wenywewe.
Hillary Clinton aliwasili kwenye mji mkuu wa Libya wa Tripoli, akiwa katika ziara ambayo haikutarajiwa. Wakati huohuo mapambano makali yanaripotiwa kuendelea mjini Sirte alikozaliwa Kanali Gaddafi. Sirte ni ngome yake ya mwisho muhimu iliyosalia.
Mwandishi: Mwadzaya,Thelma-ZPR