1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton kutoa ushahidi sakata la Epstein

17 Februari 2026

Clinton atafika mbele ya kamati ya bunge ya uchunguzi wa sakata la mtuhumiwa wa mtandao wa unyanyasaji wa kingono Jeffrey Epstein,na asisitiza wote waliotajwa lazima watoe ushahidi

Hillary Clinton waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani
Hillary Clinton waziri wa zamani wa mambo ya nje wa MarekaniPicha: Dwi Anoraganingrum/Panama Pictures/picture alliance

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje nchini Marekani Hillary Clinton ameonesha kutilia mkazo msimamo wake kuhusu sakata la mtuhumiwa wa unyanyasaji wa kingono, Jefrey Epstein, akidai watu wote waliotakiwa kutoa ushahidi , akiwemo Andrew, mwanawe hayati malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza, wanapaswa kufika mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kadhia hiyo.Mshirika wa Epstein Maxwell aomba msamaha kwa Trump kabla ya kutoa ushahidi

Clinton ambaye pia ni mkewe rais wa zamani Bill Clinton anatarajiwa kufika mbele ya kamati hiyo tarehe 26 mwezi huu kutowa ushahidi wake, siku moja kabla ya mumewe.

Clinton amekuwa akiishinikiza serikali ya rais Donald  Trump kuchapisha nyaraka zote zilizobakia kuhusu sakati la Epstein.

Wote wawili wametaka kikao cha kusikilizwa ushahidi wao kifanyike hadharani badala ya faragha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW