1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HIROSHIMA : Kumbukumbu ya miaka 60 ya shambulio la nuklea

6 Agosti 2005

Wakaazi wa Hiroshima leo wamekuwa na kumbukumbu ya miaka 60 ya kushambuliwa kwa bomu la nuklea shambulio la kwanza duniani lillilogharimu maisha ya zaidi ya watu 140,000.

Kengele ililia saa mbili na robo asubuhi na mji huo ukabaki kimya kwa dakika moja kukumbuka wakati huo Marekani ilipodondosha bomu hilo mjini humo hapo mwaka 1945.

Waziri Mkuu wa Japani Junichiro Koizumi amesema Japani inaendelea kujifunga kwa amani na inapinga silaha za nuklea.Akizungumza katika kumbukumbu hizo kwenye mji wa Hiroshima uliojengwa upya amesema kwa dhamira nzito ya kutorudiwa kwa maafa ya Hiroshima na Nagasaki Japani inaendelea kubakia na katiba yake ya amani na kushikilia kanuni tatu za kupinga silaha za nuklea.

Koizumi alikuwa akikusudia taarifa ya Japani ya mwaka 1967 kwamba haitotengeneza,haitomiliki au kuruhusu kuingizwa kwenye ardhi yake kwa silaha za nuklea.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan katika taarifa iliyosomwa kwa niaba yake ameonya kwamba bila ya kuchukuliwa kwa hatua ya pamoja dunia inakabiliwa na purukusho la kuenea kwa silaha za nuklea.

Huku kukiwa na mizozo na Iran na Korea Kaskazini juu ya silaha za nuklea Annan amesema wanashuhudia kuendelea kwa jitihada za kuimarisha na kuzifanya silaha za nuklea kuwa za kisasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW