1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hitilafu ya mtandao yaripotiwa maeneo kadhaa duniani

19 Julai 2024

Hitilafu kubwa ya mifumo ya kompyuta na kukatika kwa mtandao imeshuhudiwa mapema hii katika maeneo mbalimbali duniani, shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, mawasiliano ya simu na hata matangazo ya televisheni

hitilafu ya mifumo ya kompyuta
Shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, mawasiliano ya simu na hata matangazo ya televisheni ziimeathirika kutokaan ana hitilafu ya mifumo ya kompyutaPicha: Tim Goode/empics/picture alliance

Hitilafu kubwa ya mifumo ya kompyuta na kukatika kwa mtandao imeshuhudiwa mapema hii katika maeneo mbalimbali duniani, shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, mawasiliano ya simu na hata matangazo ya televisheni kuanzia Australia, Marekani hadi Ulaya yameathirika.

Makampuni makubwa ya ndege kuu za Marekani kama Delta, United na American Airlines yamesimamisha safari zote za ndege za siku ya leo kutokana na suala la mawasiliano, hayo yamesemwa na uongozi wa shirikisho la anga nchini Marekani (FAA).

Soma zaidi. Mfumo wa TEHAMA watetereka na kuzusha kizaazaa duniani

Hapa Ujerumani, Safari za ndege zilisitishwa katika uwanja wa ndege wa Berlin Brandenburg nchini Ujerumani kutokana na tatizo la kiufundi.

Huko Uhispania viwanja vya ndege vyote nchini Uhispania vilipata hitilafu iliyopelekea kusimama kwa shughuli zao kutokana na kuathiriwa kwa mifumo ya kompyuta .

Uwanja wa ndege wa Hong Kong pia ulisema baadhi ya mashirika ya ndege yameathirika huku mamlaka yake ikitoa taarifa ambayo inahusisha usumbufu huo.

Soma zaidi. Afrika Mashariki yakumbwa na ukosefu wa mtandao wa Intaneti

Huyo ni Maria, abiria katika uwanja wa ndege wa Lisbon nchini Ureno ambapo safari za ndege zimecheleweshwa na kuahirishwa kwa sababu ya kukatika kwa mtandao.

 "Walisema mfumo wa Transavia ulikuwa na hitilafu katika ngazi ya kimataifa, hatuwezi kuondoka kwa sababu hakuna taarifa kwa hiyo wamesema tusubiri barua pepe ili kuona kama tunaweza kupaa leo au la, sijui kitu kingine chochote. "

Katika uwanja wa ndege wa Sydney huko Australia picha mbalimbali zilizochapishwa mtandaoni zinaonyesha foleni kubwa kwenye Uwanja huo.

Vyombo vya habari vyasimamisha matangazo

Kwa upande mwingine, Mashirika mbalimbali ya habari kama vile Skynews ya Uingereza na ABC la Australia yalilazimika kusistisha matangazo yao ya asubuhi kutokana na hitilafu hiyo.

Mashirika mbalimbali ya habari kama vile Skynews ya Uingereza na ABC la Australia yalilazimika kusistisha matangazo yao ya asubuhi kutokana na hitilafu hiyoPicha: DW

Kuhusu chanzo cha hitilafu hiyo, Mtaalamu wa Chuo Kikuu cha Melbourne Toby Murray amesema kuna dalili kwamba tatizo hilo linahusishwa na chombo cha usalama kiitwacho Crowdstrike Falcon.

Soma zaidi.Meta kuchunguzwa juu ya usalama wa watoto mtandaoni

CrowdStrike ni kampuni ya kimataifa inayohusika na usalama kwa jumla pamoja na usalama wa mtandao na kwamba jukwaa hilo ni maarufu kwa kubaini masuala ya udukuzi wa kompyuta na kutoa majibu, Murray alisema.

Kwa upande wake Jill Slay, Mtafiti wa usalama wa mtandao wa Chuo Kikuu cha Australia Kusini amesema hitilafu hiyo italeta athari kubwa kimataifa.

Vyanzo: AFP na Reuters

      

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW