1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaUingereza

Hitilafu ya umeme yatatiza safari uwanja mkubwa wa Heathrow

21 Machi 2025

Mamia ya safari za ndege zimefutwa leo kwenye uwanja mkubwa zaidi wa ndege barani Ulaya wa Heathrow baada ya moto uliozuka katika kituo kimoja cha kupoza umeme kusababisha kukatika kwa nishati hiyo kwenye uwanja huo.

UK Flughafen Heathrow muss wegen Stromausfalls schließen
Ndege zimeegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa HeathrowPicha: Carlos Jasso/REUTERS

Safari za mamia kwa maelfu ya abiria duniani zimetatizika baada ya ndege kushindwa kuruka au kutua kwenye uwanja huo tangu mapema leo alfajiri.

Mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa FlightRadar umesema karibu ndege 1,350 zimeathirika na hitilafu iliyotokea.

Soma pia:Mgomo mkubwa wa viwanja ndege waendelea Ujerumani 

Mashirika kadhaa yamelazimika kuwapeleka abiria waliotarajiwa kuwasili au kuunganisha safari kupitia Heathrow kwenye viwanja vingine vya ndege barani Ulaya.

Mamlaka za uwanja huo zimesema bado hazifahamu muda ambao umeme utarejea, maelezo yanayozidisha mashaka kuwa mparaganyiko wa safari utaendelea kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW