1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hoffenheim yaibwaga Dynamo Kyiv 2-0

4 Oktoba 2024

Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Hoffenheim imepata ushindi wa 2-0 dhidi ya Dynamo Kyiv katika mechi ya mashindano ya Ligi ya Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Prezero Arena.

Wachezaji wa 1899 Hoffenheim.
Wachezaji wa 1899 Hoffenheim.Picha: Uwe Anspach/dpa/picture alliance

Mabao ya Hoffenheim yalifungwa na mshambuliaji wao Adam Hlozek.

Mwakilishi mwengine wa Ujerumani katika mashindano hayo, Eintracht Frankfurt, ilipata ushindi wa 3-1 ilipokuwa ugenini huko nchini Uturuki ikicheza na Besiktas.

Soma zaidi: Bayern yaanza vyema mbio za Champions yaitandika Dinamo Zagreb 9-2

Mshambuliaji wa Frankfurt Omar Marmoush aliendeleza mwanzo wake mwema wa msimu kwa kuwa mmoja wa wafungaji wa mabao hayo matatu.

Katika ligi ya Conference, timu nyengine ya Bundesliga Heidenheim, ilipata ushindi wa 2-1 ilipokuwa ikicheza na Olimpija Ljubljana huko mjini Heidenheim. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW