1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hofu ya kuenea kwa virusi vya Corona yatanda

6 Februari 2020

Vifo vitokanavyo na virusi vya Corona vimepanda na kufikia 563, huku tukio la maelfu ya watu wanaozuiliwa katika meli za kuvinjari likizidisha wasiwasi wa kuenea kwa virusi hivyo.

BG Wuhan Rückholaktion weltweit / Polen
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Rataj

Zaidi ya watu 28,000 kwa sasa wameambukizwa nchini China wakati serikali ikijizatiti kuvidhibiti virusi hivyo licha ya kuwalazimisha mamilioni ya watu kubakia majumbani mwao katika miji mingi nchini humo.

Nchi kadhaa mpaka sasa zimethibitisha visa vya virusi hivyo, vilivyotokea katika soko la wanyamapori mjini Wuhan mwishoni mwa mwaka uliyopita.

Wakati huo huo maelfu ya watu waliokuwa katika meli za kuvinjari mjini Hong Kong na Japan wamewekwa katika karantini, ili kujua kama moja kati yao ameambukizwa au la.

Tayari watu 20 katika meli ya Diamond Princess wamegundulika kuambukizwa, huku wengine 3,700 na wafanyakazi kutoka zaidi ya mataifa 50 wamefungiwa au kuwekwa karantini katika meli ya kuvinjari iliyoko katika bandari ya Yokohama kuanzia siku ya Jumatatu usiku.

Mjini Hong Kong watu, 3,600 walifungiwa katika meli ya World Dream na kufanyiwa vipimo vya kiafya, baada ya watu watatu kupatikana na virusi vya Corona. Hong Kong imekuwa na wasiwasi maana virusi vya Corona vimeleta kumbukumbu ya virusi vingine vya SARS vinavyosababisha matatizo ya kupumua vilivyopelekea maafa ya watu 300 mjini humo na vifo vingine 349 China bara kati ya mwaka 2002 na 2003.

Awali shirika la afya ulimwenguni lilitangaza virusi vya Corona kama dharura ya afya duniani, hatua iliyosababisha serikali kadhaa kuonya kuhusu kuitembelea China na kupiga marufuku watu kuingia nchini mwao kutoka China huku mashirika kadhaa ya ndege pia yakifuta safari zake nchini China.

Taiwan, ambayo imekuwa na visa 13 vya Corona imepiga marufuku kabisa meli za kuvinjari kutia nanga katika bandari zake.

Vyanzo: afp/Reuters

 

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW