Mashirika yahofia 'maovu makubwa', uchaguzi ujao Uganda
18 Januari 2025Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80, atakuwa madarakani kwa miaka 40 wakati uchaguzi utakapofanyika Januari 12, mwaka 2026, huku akidhamiria kuwania muhula wa saba, kukandamiza upinzani na kutoa vitisho kwa yeyote anayetaka kurithi nafasi hiyo.
Wakati wa uchaguzi wa rais mwaka 2021, upinzani ulieleza kuwa mamia ya wafuasi wao walitoweka au kuuawa, huku mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa Robert Kyagulanyi maarufu kama
Soma pia: Polisi nchini Uganda yawakamata waandamanaji 104
Bobi Wine anayezingatiwa kama tishio kubwa zaidi kwa utawala wa Museveni akitaja kuwa hana matumaini yoyote kuwa uchaguzi ujao nchini Uganda utakuwa huru na wa haki.
Bobi Wine ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Museveni anafahamu kwamba serikali yake haina uhalali na haitakiwi na idadi kubwa ya watu, ndio maana amekuwa akitumia nguvu ili kuhakikisha anasalia madarakani. Ameongeza kuwa wako tayari kuendelea na mapambano ya kuikomboa Uganda bila kujali ni kwa kiasi gani watapata madhara.