1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Hofu Msumbiji kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi

20 Desemba 2024

Msumbiji inajiandaa kwa maandamano zaidi pale tangazo la matokeo ya mwisho ya uchaguzi yenye utata litakapotolewa kabla ya siku ya Jumatatu inayokuja.

Msumbiji | Maputo 2024 | Waandamanaji
Waandamanaji wanakimbia wakati wa purukushani kati yao na polisi katika kitongoji cha Luis Cabral huko Maputo, Msumbiji, Novemba 7, 2024.Picha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Msumbiji inajiandaa kwa maandamano zaidi pale tangazo la matokeo ya mwisho ya uchaguzi yenye utata litakapotolewa kabla ya siku ya Jumatatu inayokuja.

Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane ametishia kuitisha vurugu nchi nzima kama Baraza la Kikatiba litaidhinisha matokeo ya awali ambayo yalimuweka katika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Oktoba 9 akishindwa na mgombea wa chama tawala cha Frelimo.

Soma pia: Mondlane atishia kuanzisha vurugu kubwa Msumbiji 

Msumbiji imekumbwa na miezi miwili ya ghasia ambazo zimewauwa watu 130 na kusababisha uharibifu mkubwa. Aidha vurugu hizo za baada ya uchaguzi zimekwamisha shughuli za kibiashara mijini, na kuathiri uzalishaji viwandani.

Serikali ya Marekani jana iliongeza tahadhari yake ikionya dhidi ya safari za kwenda Msumbuji, ikisema maandamano yanaweza kugeuka haraka na kuwa fujo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW