SiasaHonduras
Honduras na China kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia
26 Machi 2023![China I China und Honduras nehmen diplomatische Beziehungen auf](https://static.dw.com/image/65123805_800.webp)
Matangazo
Tangazo la China kuhusu hatua hiyo linajiri muda mfupi baada ya Honduras kusema kuwa imesitisha rasmi uhusiano na Taiwan, ambayo imepoteza washirika kadhaa wa Amerika Kusini katika miaka ya hivi karibuni.
Mabadiliko hayo, yanaripotiwa siku chache tu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Enrique Reina kufanya ziara mjini Beijing, na kuiacha Taiwan ikiwa na nchi 13 tu zinazoitambua rasmi kuwa huru.
Soma pia: China imerejelea vitisho vya kuishambulia Taiwan
Waziri Reina amesema Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa kunako eneo la China.