Haki za binadamuHong Kong
Hong Kong yafutilia mbali pasi za usafiri za wanaharakati
12 Juni 2024Matangazo
Msemaji wa serikali hiyo amesema wanaharakati hao sita ambao wote wako kwenye orodha iliyotolewa na serikali ya wanaharakati 13 wanaotafutwa, wanajificha nchini Uingereza.
Mbali ya kufutilia mbali pasi zao za usafiri, polisi ya Hong Kong imesema kuwa mtu yeyote anayewafadhili au kufanya biashara nao, anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka saba jela.
Tangu mamlaka zipige marufuku maandamano ya kupigania demokrasia mwaka 2019, Hong Kong imezidisha kamatakamata dhidi ya wapinzani na kuweka sheria kali, ambazo wakosoaji wake kama Uingereza na Marekani wanasema, zimebinya uhuru wa kipekee iliyokuwa nao sehemu hiyo ya China.